Kwa APS - Namna ya kuhakikisha ufuatiliaji wa waliookoka katika ukatili wa kijinsia

Kiisha  mashauri ya kwanza, lazima yule yule aliye kumbwa na vitendo vya uwaki arudi kwa munganga  ndani ya muda unayowekwa hapa chini lakini pia ndani ya mipango  ya APS:

 Hakikisha ufuatiliaji huku ukiheshimu mwendo, mahitaji yanayofaa pamoja na tarehe za mwisho zinazohitajika kwa kila kesi:

 

a.  Wiki 2 baada ya matibabu ndani ya masaa 72: 

Mwathirika anarudi kwenye kituo cha afya kwa:

Kwa APS ni : 

  • Tawala fujo za zamani: Cunguza  hali ya kiakili, matendo ,tabia , tambua  uwezo yenye iko na utoe usaidizi wa kisaikolojia 
  • Omba kipimo cha  ujauzito ikiwa haujafanywa wakati wa matibabu ya kwanza 
  • Omba  kipimo cha VVU ikiwa hakijafanywa wakati wa matibabu ya kwanza
  • Toa matibabu mengine ya ARV kama ni lazima 
  • Fanya uchunguzi wa kimatibabu kwa magonjwa ya zinaa na ufanyie uchunguzi wa kimatibabu ikiwa ni lazima

b.  Mwezi wa kwanza kisha matibabu ndani ya masaa 72.

Mwathiriwa atarudi kwenye kituo cha afya kwa:

Kwa APS ni : 

Kuangaliya  hali ya kihisia, tengeneza mifumo ya kukabiliana na kijamii na mitazamo pamoja

  • Kutoa kipimo cha pili cha dawa (Chanjo ya hapatitis na pepopunda)
  •  Ku shauri kipimo ya ujauzito kama haikufanyika kwa usaidizi wa kwanza.
  • Kufanya vipimo vya matibabu na vya uchunguzi kwa magonjwa ya zinaa
  •  Kushauri vipimo vya VVU kama haikufanyika kwa usaidizi wa kwanza

c. Mwezi wa 3 kisha matibabu ndani ya ma saa 72.:

Kwa APS ni : mwaziriwa anarudi kwenye kituo cha afya kwa: 

  • Kuchunguza hali ya kisaikolojia ya SVBG na ujuzi wa maisha.
  • Kwa kesi ya ujauzito na kama mwaziriwa anakubali kuchunga ujauzito wake, kumuongoza kwenye vipimo vya wajawazito (CPN), na kama mwaziriwa anakataa kuchunga ujauzito wake, kumuongoza kupitiya shurti na mwongozo ya matunzo kamilifu ya utoaji mimba kama vile inatakiwa kwa wanawake katika inchi yetu RDC(SCACF)
  •  Wakati vipimo ya VVU vimeonyesha kuwepo kwa ugonjwa, fuata kanuni ya usaidizi.
  •  Wakati vipimo vya VVU havionyesha kuwepo kwa ugonjwa, rudiliya tena vipimo kisha myesi 3, kisha myezi sita na kisha myezi 12
  • Kwa magonjwa ya zinaa, fanya vipimo vya matibabu na vya ucunguzi.

d.  Katika mwezi wa 6 baada ya matibabu ndani ya masaa 72: 

Mwazirika anarudi kwenye kituo cha afya kwa  :

Kwa APS : 

  • Ku cunguza  hali ya kihisia  na kujaza  ki kartasi  ca kuzuia kurudi tena kwa magonjwa ikiwa kuna maendeleo.
  • Rudiliya  mpango  wa usaidizi wa kisaikolojia ikiwa hakuna maendeleo 
  •  Toa vipimo vya kuchunguza VVU na ushauri  kama hili halijafanyika, hakikisha kwamba ushauri  unatolewa kabla na baada ya kupima na uwaongoze kwenye  huduma za ECP (kinga, matibabu na matunzo) za VVU/UKIMWI.

e. Katika mwezi wa 12 baada ya matibabu ndani ya masaa 72: 

Mwazirika anarudi kwenye kituo cha afya kwa:

Kwa APS : 

  • Kuchunguza  hali ya kihisia 
  • Toa kipimo cha VVU ikiwa hapo mbele  haikuonekana  au kama hakijafanyika
  • Ongoza kwenye  mupango  ya usaidizi wa kisaikolojia na kijamii ikiwa haujafanywa wakati wa mipango  iliyopita. Njia  zaa ubora Kuheshimu haki za mteja, Umuhimu, kuendeleya, Maelewano, siri, Njia  zaa kuchunguza matokeo  Heshimu taratibu ya utendaji, Ripoti ya Ufuatiliaji