Msaada wa jamii - Namna ya kuhakikisha ufuatiliaji wa waliookoka katika ukatili wa kijinsia
Kiisha mashauri ya kwanza, lazima yule yule aliye kumbwa na vitendo vya uwaki arudi kwa munganga ndani ya muda unayowekwa hapa chini lakini pia ndani ya mipango ya APS:
Hakikisha ufuatiliaji huku ukiheshimu mwendo, mahitaji yanayofaa pamoja na tarehe za mwisho zinazohitajika kwa kila kesi:
a. Wiki 2 baada ya matibabu ndani ya masaa 72:Msaada wa jamii unapaswa kufanya nini miezi 3 baada ya yule aliye kumbwa na uwaki kuondoka kwenye kituo cha afya:
Fuatilia ikiwa mwaziriwa alirudi kweli kwenye kituo cha afya
Kucungaza kama kweli mwaziiriwa alitumia dawa kama vile inaitajika.
Kucunguza kama hakuna shida mwaziiriwa alipata kupitiya kutumiya dawa.
b. Mwezi wa kwanza kisha matibabu ndani ya masaa 72.Msaada wa jamii unapaswa kufanya nini wiki 4 baada ya mwazirika kuondoka kwenye kituo cha afya:
Fuatilia ikiwa mwaziriwa alirudi kweli kwenye kituo cha afya
Kucungaza kama kweli mwaziriwa alitumia dawa kama vile inaitajika.
Kucunguza kama hakuna shida mwaziiriwa alipata kupitiya kutumiya dawa.
Ku harifu APS kuusu ujiyo wa mwaziiriwa kwenye kituo cha afya.
c. Mwezi wa 3 kisha matibabu ndani ya ma saa 72.: Msaada wa jamii unapaswa kufanya nini myezi 3 baada ya mwazirika kuondoka kwenye kituo cha afya:
Fuatilia ikiwa mwathiriwa alirudi kweli kwenye kituo cha afya
Kusikiliza mwathiriwa kama anaweza kuwa na shida ingine
Ku harifu APS kuusu kufika kwa mwathiriwa kwa mafunzo ya Afya.
d. Katika mwezi wa 6 baada ya matibabu ndani ya masaa 72:Msaada wa jamii unapaswa kufanya nini miezi 6 baada ya mwazirika kuondoka kwenye kituo cha afya:
Fuatilia ikiwa mwathiriwa amerejea kwenye kituo cha afya
Msikilize aliyenusurika. ikiwa kuna shida nyingine.
Mwishoni ripoti APS ya kuwasili kwa mwathirika katika kituo cha afya.
e. Au Katika mwezi wa 12 baada ya matibabu ndani ya masaa 72:Msaada wa jamii unapaswa kufanya nini miezi 12 baada ya mwathirika kuondoka kwenye kituo cha afya:
Fuatilia ikiwa mwaziriwa amerejea kwenye kituo cha afya
Msikilize aliye pitiya vitendo vya uwaki. ikiwa kuna shida nyingine.
Mwishoni ripoti APS juu ya kufika ya aliyeokoka ku kituo cha afya.Wakati wowote mwazirika anapokuja kukutana na msaidizi wa jamii, Nini cha kufanya na mtazamo wa kuchukua
Nini cha kufanya :
Kumkaribisha aliye tendewa uwaki.
Jitambulishe tena
Hakikisha kama kuko burafiki bwa karibu.
Hakikisha kama ni salama kwa aliyeokoka kuzungumza nawe kwa wakati huu
Sema kazi yako yenye ni kuelewa shida yao ya sasa na kuchungu umuhimu wa kuongoza kwenye kituo ca afya.
Eleza yanao angaliya usiri na mipaka yake
Eleza haki zao (mnusurika anaweza kuacha, kukataa kujibu, kuuliza maswali)
Eleza jinsi habari zitachungiwa
Muulize kama ana maulizo yoyote
Muombe ruhusa ya kuendelea
Mtazamo
Kueshimiya kanuni zenye zinaongoza:
Haki ya usiri. Maelezo ya aliyeokoka haisemeki bila ruhusa
Haki ya usalama: Usalama wa kimwili na kihisia ya aliye okoka lazima uhakikishwe wakati wote wa usaidizi
Haki ya utu na kujitawala: Maoni na maamuzi ya mtu aliyeokoka yanaheshimiwa na kufuatwa kwa vile vilivyo.
Kutobagua: Kila aliyeokoka hupokea matibabu na huduma sawa
Hali ya sura yenye inafaa.
Onyesha sura ya furaha.
Sauti ya upole
Onyesha mambo mengine ya asili..
kama ni mtoto, ji shushe mpaka ku kimo yake.
Mutege sikiyo (usipokee simu, n.k.)
Usimkate wakati iko nasema; mpe muda wa kuongea
Tumikisha luga ya heshima
Usilaganishe byenye hauta weza kufanya.
Sema habari ya kweli na ya ku aminika
Fuata: fanya kile unachosema utafanya
Usimwambie mtu kile “anachopaswa” kufanya, na mpe taarifa za kumsaidia kufanya byenye anakusudiya yee peke.