Nini utafanya saa yote yenye unapokeya kesi ya aliyeokoka?

  Wakati wowote unaweza kumpokea aliyeokoka  ambaye hata ameruhusiwa na kituo cha afya mwenye anarudi kwako  na iko na  matatizo. Itakuwa muhimu kwako kuongozana  naye na kuzungumza 

.
Hajitunzi yeye mwenyewe wala watoto wake, jambo ambalo linamtenga zaidi

 Ifanyike na musaada wa jamii

  • Mu hakikishie aliyeokoka
  • Wasiliana na APS haraka
  • Umuonyeshe  na/au umusindikize  aliyeokoka  kwa kituo cha afya
    .
    Aliyeokoka   anashindwa kupata marafiki wake wa zamani  ao  kanisa 
  • Tengeneza njia  pamoja nao yenye  itawasaidia kuungana tena na mahusiano  mazuri (kwa sababu mojawapo ya njia bora za walio okoka  kupona ni kurudia ku kazi  zabo za kila siku,
  •  Chukua  muda kufanya shughuli zinazojenga matumaini na kuwapa nguvu na ujasiri, na kuwa karibu  na watu wanaowatia moyo na kuwaunga mkono. )
  • Kama iyi inakushinda: mpeleke aliye okoka  kwenye mipango  kamili  ambazo shirika lako hutoa, kama vile vipindi vya usaidizi wa kikundi, mipango  za mafunzo ya kazi za mikono.
    .
    Hatumikake tena,

Hatokake  mu nyumba  tena,

Hazungumzake  tena na familia yake na marafiki, ao  kuwaona tena, 

Ana shida ya kulala ao ana  lala sana, 

Malalamiko ya maumivu ya mwili (maumivu ya tumbu, maumivu ya mishipa, maumivu ya kichwa);  

Amebadilisha mazoea yake ya kula (kula sana au kula kidogo), anakuwa wa  huzuni mara mingi, Anaonyesha  kukosa matumaini kuhusu hali yake au maisha yake.

fanyike  na msaada  wa jamii

  • Muhakikishie aliyeokoka
  •  Wasiliana na APS haraka
  • Mu onyeshe  na/ao  umusindikize  aliyeokoka  kwa kituo cha afya
    .
    Iko na  mawazo ya kujiua na kutaka kupita kwa tendo, 
    Ifanyike  na msaada  wa jamii
  • Kutoa taarifa ni  shurti
  • Kuangaliya   usalama;
  •  Weka "zamu  wa usalama"
  • Wasiliana / elekeza.